BAKARI Mwamnyeto, nahodha wa Coastal Union amesema wamejipanga kulipa kisasi
kwa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa leo Uwanja wa Mkwakwani.
Kwenye mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo Uwanja wa Uhuru jijini Dar,
Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Abdulaziz Makame.
Coastal
Union inaingia katika mchezo huo ikiwa na maumivu ya kufungwa mabao 2-1 na
Ruvu Shooting,Yanga ikitoka kuambulia sare ya 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania.
“Tunafahamu mchezo
utakuwa mgumu ndani ya dakika zote tisini kutokana na presha ya mashabiki wa
pande zote mbili, lakini tumejipanga kulipa kisasi, hatutaki kuona tunafungwa
tena na Yanga,” amesema beki huyo.







0 COMMENTS:
Post a Comment