MARCEL Kaheza, mshambuliaji wa Polisi Tanzania amesema kuwa malengo yake makubwa ni kucheza soka la kulipwa nje ya nchi ili kutimiza ndoto zake.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kaheza amesema kuwa amekuwa akipambana kwa ajili ya kutimiza ndoto hizo jambo ambalo huwa haachi kuomba kila awapo uwanjani na nje ya uwanja.
"Kuna mengi ya kufanya kwenye mpira na sasa ninapambana kwa ajili ya kutimiza ndoto zangu za kucheza nje ya nchi, wakati upo na nina amini kila kitu kinawekezana.
"Kila siku kabla ya mazoezi na baada ya mazoezi huwa ninamuomba Mungu ili anipe kibali katika yale ninayoyafanya, juhudi bila kukata tamaa ni vitu ambavyo ninafanya siku zote," amesema.
Kaheza alikuwa Kenya akiitumikia Klabu ya AFC Leopards alipelekwa kwa mkopo akitokea Simba kwa sasa yupo ndani ya Polisi Tanzania iliyo chini ya Malale Hamsini.








0 COMMENTS:
Post a Comment