IMEELEZWA kuwa sababu kubwa ya ushindi mfululizo kwa wachezaji wa Simba ni kufuata maelekezo ya mwalimu pamoja na kushirikiana ndani ya timu.
Simba imeshinda mechi nne mfululizo mara baada ya kutoka kuonja joto ya jiwe mbele ya JKT Tanzania kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru.
Ilianza kushinda mabao 3-0 mbele ya Mtibwa Sugar, ikashinda bao 1-0 mbele ya Lipuli, ikashinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar na kumalizia mbele ya Biashara United mabao 3-1.
John Bocco, nahodha wa Simba amesema kuwa kinachowabeba wachezaji na timu kiujumla ni ushirikiano.
"Kuna kazi moja ambayo tunayo kutafuta matokeo ndani ya uwanja hali hiyo inatufanya tushirikiane na kupambana kwa juhudi jambo linalotupa matokeo mazuri,".
Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 62 baada ya kucheza mechi 24 inafuatiwa na Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi zake 45.







0 COMMENTS:
Post a Comment