February 25, 2020


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa wanadai ameipunguzia kasi ya kuuwinda ubingwa Azam FC baada ya kulipa kisasi kwa kuifunga bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Majaliwa jambo ambalo halielewi.
Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Chamazi, Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba iliinyoosha kwa mabao 2-1 Namungo, kwenye mchezo wa pili Azam FC iliacha pointi tatu Uwanja wa Majaliwa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa hajali kama ameipunguzia timu hiyo kasi ya ubingwa yeye anafurahi kuifunga timu kubwa na ngumu ikiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.
“Wanasema nimewapunguzia kasi ya ubingwa mimi sijui, ninachojua timu yetu ya Namungo imeongeza pointi tatu na imeshinda mbele ya timu ngumu ambayo ilitufunga kwenye mechi yetu ya kwanza nasi tumewapa kilichostahili kutokana na makosa yao,” amesema Thiery.
Bao pekee la ushindi kwa Namungo lilifungwa na nahodha ambaye ni mzawa mwenye mabao mengi kwa sasa Reliats Lusajo mwenye mabao 10 kwenye orodha ya wafungaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic