February 24, 2020

KOCHA Mkuu wa Tanzania Prisons, Adof Rishard amesema kuwa anaridhishwa na uwezo wa wachezaji wake ndani ya uwanja kutokana na kufanya kile anachowaelekeza.

 Prisons jana imeshinda mabao 2-0. Mabao ya Prisons yalifungwa na beki Salum Kimenya dakika ya 12 na Ismail Aziz dakika ya 90.

Rishard amesema:-"Ninakubali kile ambacho wachezaji wangu wanakifanya uwanjani, huwa ninawaambia kwamba ni lazima wapambane ili kupata matokeo kwani ushindani ni mkubwa na ligi ni ngumu,".

Prison ipo nafasi ya tisa ikiwa na pointi 33 imecheza mechi 24 huku Lipuli ikiwa nafasi ya 12 pointi 29 imecheza mechi 24.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic