UONGOZI wa Coastal Union ya Tanga umeandika waraka huu kwa mashabiki wao kuhusu tukio la Ofisa Uhamasishaji Antonio Nugaz kudai kuwa alitaka kuibiwa simu na mashabiki wa Coastal Union wakati Yanga ikicheza ja Coastal Union:-
Wapenzi wa Coastal Union pamoja na mashabiki wote wa soka tunaomba tutoe ufafanuzi juu ya tukio la vurugu lililotokea katika jukwaa la VIP likimhusisha Afisa Mhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz na shabiki mmoja.
Kilichotokea ni kwamba Nugaz alikuwa akiwalalamikia baadhi ya viongozi wa Coastal Union kwamba tumefungwa na Ruvu Shooting lakini wao tumewabania na pia kwa mujibu wake alilalamika kuwa mwamuzi hakuwa fair kwao.
Wakati anaongea shabiki anayedaiwa kutaka kumwibia simu yake alikuwa anamrekodi anachoongea jambo ambalo Nugaz hakutaka na kuanza kulumbana kutaka apewe simu ili ifutwe kile kilichorekodiwa na kusababisha taharuki lakini si kweli kwamba yule shabiki alikuwa mwizi.
Kusema hivyo tunaomba kuwaeleza mashabiki wa soka wanaotaka kuja kutazama mpira uwanja wetu wa nyumbani wa Mkwakwani wasiwe na hofu hakuna wezi na kuna usalama wa kutosha.
MIMI NIMECHEZA MPIRA UWANJA WA MKWAKWANI NIKIWA NA TIMU YA AFRICAN SPORTS MWAKA 1988/89,WIZI HAPO NI KITU CHA KAWAIDA SANA HATA MAREHEMU BWANA KAKA ALIKUWA AKILALAMIKA SANA ENZI ZILE.
ReplyDeleteWizi uko popote mpka misikitini na makanisani tatizo Hilo tukio alidanganya hakusema ukweli hakutaka kuibiwa sim
DeleteWizi wa nini?Wacha uzushi akiendekea tutatoa klipp iliyorekodiwa.Bwana Kaka alikuwa anakaa majukwaani?Wacheni uzushi.Alikuwa anajaribu kuzima focus ya kutoka sare.
ReplyDelete