February 26, 2020


FREDRICK Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa wana sababu kubwa sita zinazowafanya washinde leo mbele ya Gwambina mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa leo saa 10:00 Uwanja wa Uhuru mshindi atakayepenya leo anatinga hatua ya robo fanali.

Mwakalebela amesema:-" Tuna kila sababu ya kuifunga Gwambina kwa sababu tuna benchi la ufundi zuri, wachezaji imara, mbinu kali, uwezo mkubwa, nia ya kufanya vizuri ipo.

"Pia kuifunga Gwambina kutaturejesha kwenye mstari wetu ambao tulikuwa kwani hatukuwa na matokeo mazuri  na itatufanya turudishe imani kwa mashabiki wetu hivyo ushindi wetu mbele ya Gwambina ni muhimu mashabiki mjitokeze kwa wingi," amesema.


1 COMMENTS:

  1. Tuiikazeni leo tusifungwe au Kutoka droo kwakuwa wanaotowa mabilioni Yao tutawavunnja moyo ikiwa hapana maendeleo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic