February 21, 2020


FRANK Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea kwenye kibarua chake kesho dhidi ya Spurs amekuwa na wasiwasi wa kutowatumia baadhi ya nyota wake muhimu ambao ni majeruhi.

Wachezaji hao ni pamoja na N'Golo Kate, Ruben Loftus-Cheeck, Christian Pulisic, Tammy Abraham,Callum Hudson Odoi na Andreas Christensen.

Jose Mourinho bosi wa Spurs huenda atakosa huduma za nyota wao ambao ni Harry Kane ambaye ni majeruhi wa muda mrefu, Son Heung-min aliumia kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa.

Kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa ya Mbwana Samatta ambapo walishinda kwa mabao 3-2 imeripotiwa kuwa atakaa nje ya uwanja wiki sita hadi 12 kutokana na kuvunjika mkono.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic