February 22, 2020


KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Abadlaah Mohamed 'Bares' leo atakuwa na kazi mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

JKT Tanzania ipo nafasi ya saba ikiwa imecheza mechi 23 imejiwekea kibindoni pointi 35.

"Kazi ni moja tu kufanya vizuri na kupata pointi tatu zitakazotufanya tufike malengo tuliyojiwekea, wachezaji wapo vizuri na nina imani watafanya kazi nzuri uwanjani.

"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao kwani wana umuhimu kwenye mechi yetu," amesema.

Mchezo wao uliopita JKT Tanzania ililazimisha sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar iliyo chini ya Zuber Katwila.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic