February 23, 2020


KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone amesema kuwa anafurahi kufunga bao lake la kwanza ndani ya Simba na malengo yake ni kuisiaidia timu yake hiyo.

Luis jana kwenye ushindi wa mabao 3-1 Uwanja wa Taifa mbele ya Biashara United alihusika kwenye mabao mawili ambapo alifunga bao la kwanza dakika ya 35 kwa pasi ya Jonas Mkude na alitoa pasi kwa Meddie Kagere huku lile la tatu likifungwa na Francis Kahata.

Luis amesema:-"Ninafurahi kutupia bao ndani ya Simba, kikubwa ambacho nafikiria ni kuona kwamba ninaipa ushindi timu kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu na hilo linawezekana,".

Lusi alijiunga na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea timu ya UD Songo.

7 COMMENTS:

  1. huyu jamaa ni nooma sana Umetisha kaka

    ReplyDelete
  2. Wacha tu watanzania tujiaminishe kuwa Ndemla ana kipaji? Ila turudi pale pale vijana wetu nna maana ya wachezaji wetu wamelala mno katika kuchangamkia fursa. Hao akina Ajibu,Rashid Juma.Sisemi kuwa ni wachezaji wabaya ila tabia ya kitanzania ya kusubiri kuchangamkiwa na fursa badala ya kuzichangamkia ni tatizo na linatuchelewesha kupiga hatua ya maendeleo yetu binafsi na Taifa.Mechi mbili tu Louis Miquissonne tayari maeshaonesha kuwa ni zaidi ya kipaji. Hakuna kipya ninachokiona kwa Louis isipokuwa anafurahia kazi yake,anajiamini kweli kweli katika maamuzi bila kufikiria kocha kaniambia nini cha kufanya,na kikubwa zaidi nilichokiona kutoka kwa Louis Miquissonne ni kule kuithamini kila touch anayoipata anapopata mpira kudhamiria kufanya mambo makubwa na anafanya. Hakika kwa Miquissonne huyu Simba walikuwa lazima waondolewe tu kwenye klabu bingwa Africa. Fikiria kama Miquissonne angekuwa ni mchezaji wa Biashara kwenye hii mechi halafu uniambie kama Simba wangekuwa na nafasi ya ushindi? Uongozi wa Simba lazima ujitafakari hasa ule unaojihusisha na usajili kwani mara nyingi huwa kama wanakurupuka. Kimsingi tangu Simba watolewe klabu bingwa Africa hakuna mchezaji aliesajiliwa mwenye uwezo wa kuja kukiongezea nguvu kikosi kuvuka hatua ya robo faianal isipokuwa ndio sasa watanzania na wanasimba tunaweza kujiridhisha kwa kusema kuwa huyu Lousi ni moja kati ya ingizo bora kabisa ndani ya Simba. Na sio kama wachezaji hawapo wenye uwezo, la hasha wachezaji wapo wengi tu Africa ila naamini kuna kajiuzembe fulani ndani ya simba kwa wenye kushughulikia usajili. Tulishasema mara nyingi Boko/kagere ni wachezaji wazuri lakini pia ukizerejea video za Simba kuangalia scoring performance ya mchezaji mmoja mmoja hasa kwenye eneo la fowadi utagundua kuwa kuna upotevu mkubwa wa nafasi za wazi za kufunga kutoka kwenye uwili huu na kiasi fulani utaona uongozi wa Simba kama wameridhika na kuamini kuwa hawana uwezo wa kupata fowadi bora na wenye uwezo zaidi ya Boko kagere? Point ni kwamba ni lazima asajiliwe fowadi mwengine mwenye uwezo zaidi ya hawa wawili na hiyo ndie njia pekee ya kuipeleka Simba kutoka kwenye hii level ya sasa na kwenda another level na kuleta ushindani zaidi hasa klabu bingwa Africa.

    ReplyDelete
  3. ajitahidi kutulia na kucheza kwa malengo, zaidi sana aongeze mazoezi kupata pumzi inayoendana na uchezaji wake maana anatumika sana una wakati unaona kabisa pumzi imekata..........hii itamsaidia kucheza mahali popote maana inaonekana kutotulia kwake ndio kunamanya aonekane yuko too mechanical than clinical

    ReplyDelete
  4. Anajua sana, na anajituma sana aka anaipenda kazi yake

    ReplyDelete
  5. Baada ya season moja mikisone atajiishia zake kama kagere

    ReplyDelete
    Replies
    1. ndio atajiishia lakini atakuwa tayari kayanya yake yaliyombidi kuisha ni hali ya kawaida hata kante tayari ndo anaelekea lakin kafanya yake yaliyokuwa yanamhusu

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic