February 21, 2020


UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa umetumia gharama kubwa kukodi Uwanja wa kufanyia mazoezi kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa kuchezwa kesho Uwanja wa Sokoine.

Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru amesema kuwa wameshindwa kuutumia Uwanja wa Sokoine baada ya kuwakuta wenyeji wao wakiutumia.

"Tumeshindwa kuutumia Uwanja wa Sokoine baada ya wenyeji wetu Mbeya City kuutumia, imetugahrimu pesa nyingi kukodi uwanja mwingine wa mazoezi.

"Ombi langu kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulitazama hili kwani halipo kwenye kanuni ni lazima mgeni acheze kwenye uwanja wa mechi siku moja kabla ya mchezo," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic