February 5, 2020


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga, raia wa Ubelgiji leo atakabiliwa na mtihani wake wa sita ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kucheza na timu yenye safu kali ya ushambuliaji kushinda yake ndani ya Ligi Kuu Bara.
Mbelgiji huyo ameiongoza timu yake kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar na ilichapwa mabao 3-0, Azam 1-0 Yanga, Singida United 1-3 Yanga,Yanga 1-0 Mtibwa Sugar, Yanga 2-0 Tanzania Prisons huu ulikuwa wa Shirikisho.
Eymael anamtegemea David Molinga mwenye mabao sita huku Lipuli ikiwatazama vijana wake wawili wazawa ambao ni Paul Nonga na Daruesh Saliboko ambao wote wametupia mabao nane nane kila mmoja.
Kocha Mkuu wa Yanga aliliambia Championi Jumatano kuwa kinachowashinda washambuliaji wake ni kushindwa kufanya maamuzi jambo linawafanya washindwe kufunga.
“Nina mechi nyingi ngumu ambazo ninapaswa nishinde ikiwa ni pamoja na mechi yetu dhidi ya Lipuli ila tatizo wachezaji wangu wanashindwa kufanya maamuzi ya haraka wakiwa ndani ya 18 jambo linalotufanya tusifunge mabao mengi,” alisema.

2 COMMENTS:

  1. Lipuli ni kati ya timu zinazokamata mkia na Hakuna haja ya kusherehekea ushindi kwa kujiona mbabe kwa kuifunga timu kama hiyo

    ReplyDelete
  2. mimi naona ni tahadhari hapo na wala sioni sherehe ya ushindi !! ushindi upi wakati mechi haijachezwa????

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic