February 15, 2020


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa uwepo wa David Molinga ndani ya Yanga ni moja ya silaha kwake itakayompa ushindi kwenye mechi zake zote.

Molinga ni kinara wa utupiaji ndani ya Yanga akiwa na mabao 7 anafuatiwa na Patrick Sibomana mwenye mabao manne na asisti moja.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Eymale alisema kuwa amezungumza na Molinga kuhusu tatizo lake la kukosa utulivu jambo litakalompa nafasi ya kufunga mabao mengi na kutengeneza nafasi kwanye mashindano watakayoshiriki.

“Tuna kazi kubwa ya kufanya kwa kuwa wapinzani wetu wanazidi kujipanga hilo tunalitambua na tunalifanyia kazi, kwa uwezo ambao anaouonyesha Molinga atafunga mabao mengi, jambo litakalofanya mashabiki wafurahi,” alisema.

Yanga imefunga jumla ya mabao 24 katika Ligi Kuu Bara ikiwa imecheza jumla ya mechi 19 ipo nafasi ya tatu na pointi 38, mchezo unaofuata ni dhidi ya Tanzania Prisons, leo Jumamosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic