KIGI Makasi nahodha wa Ndanda FC amesema kuwa wachezaji wana morari kubwa ya kuzitafuta pointi tatu kwenye mechi zake zote zinazofuata ili kujiokoa kwenye nafasi ya kushuka daraja.
Ndanda FC ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona, leo itakuwa kibaruani kumenyana na KMC.
"Kazi kubwa ni kuona tunapata pointi tatu mbele ya wapinzani wetu wanaokuja hapa Nangwanda, tutapambana kupata pointi tatu ili kubaki kwenye ligi msimu ujao nafasi ipo," amesema.
Ndanda ipo nafasi ya 15 ikiwa imecheza mechi 22 ina pointi 23 wapinzani wao KMC wapo nafasi ya 17 na pointi zao 21.








Mnakumbuka shuka wakati kumekucha
ReplyDelete