PAPY Tshishimbi nahodha wa Yanga amepewa jukumu la kuwaongoza wachezaji wenzake wageni pamoja na kikosi cha Yanga kwenye mechi zote za mikoani ambazo timu yake itacheza.
Imeelezwa kuwa wachezaji wengine wageni ambao watafanya kazi kwa ukaribu na Tshishimbi ni pamoja na Haruna Niyonzima, Lamine Moro, Shikhalo na Bernard Morisson kutokana na kuonyesha kiwango kilichokubalika ndani ya benchi la ufundi linaloongozwa na Luc Eymael.
Wachezaji hao wote ambao ni wageni imeelezwa kuwa wamepitishwa na Kocha Mkuu Eyamel kucheza kwenye viwanja vya mikoani kutokana na kumudu ushindani wa ugumu wa viwanja vya mkoani.
"Benchi la ufundi limekubaliana baada ya kufanya tathimini kwenye mechi dhidi ya Polisi Tanzania na kupata wachezaji wanaoumudu viwanja vya nje ya Dar.
"Kikubwa walichokubaliana ni kuwatumia wachezaji wazawa ili kuwapa nafasi kutumia uzoefu kwenye viwanja vya nyumbani walivyovizoea,". Imeeleza taarifa hiyo.
Yanga leo ina kibarua cha kutafuta pointi tatu mbele ya Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kikubwa ambacho wanakifanya kwa sasa ni kujenga timu yenye ushindani itakayopata matokeo kwenye mechi zake zinazofuata.








bado MNAJENGA TIM ilihali ligi inaelekea ukingoni? mpate funzo la kubadili kocha na kuakanya 11 eleven msimu mzima
ReplyDeleteUbingwa tulisha weka pembeni,kwani tunahitaji muujiza kuweza kutwaa ubingwa, acha tujenge kikosi maana kocha mgeni na kuna baadhi ya wachezaji wageni.
DeleteKubadilisha mocha sio tatizo, mbona hata Simba wamebadili kocha ktk ya msimu.
ReplyDeleteWacha na wao Yanga wajenge kikosi ndio soka, haiwezekani kila msimu mukawa team Bora.