February 15, 2020


Paul Pogba anataka kuondoka Man United mwisho wa msimu huu lakini fursa ya mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 kuweza kuondoka vizuri katika klabu hiyo huenda zikaathiriwa na hatua ya klabu hiyo kuomba kulipwa £83m ili kumuuza nyota huyo (Guardian)

Manchester United imeajiandaa kuwanunua wachezaji watatu wa England iwapo itafanikiwa kumuuza Pogba - kiungo wa kati wa Leicester James Madison, kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish, 24, na mshambuliaji wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19. (Star)

Maddison anataka kujiunga na Manchester United. (Manchester Evening News)

Klabu za Arsenal na Chelsea zinafikiria kuwasilisha ombi la kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania mwenye thamani ya £63m Isco, 27, huku klabu ya Real Madrid ikitafuta kuchangisha fedha kujiandaa kwa dirisha la uhamisho la mwisho wa msimu huu. (Sun)

Ligi ya Premier League itaendeleza uchunguzi wake dhidi ya Manchester kufuatia hatua ya shirikisho la soka Ulaya Uefa kuwapiga marufuku kushiriki katika mechi za ligi ya mabingwa kwa misimu miwili mfululizo. (Mirror)

Manchester City huenda ikapunguziwa pointi moja katika ligi ya England na huenda pia ikalazimishwa kucheza katika ligi ya pili kufuatia hatua yake ya kupigwa marufuku, wataalama wameonya. (Star)

Arsenal na mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, watelengwa na Inter Milan iwapo klabu hiyo itampoteza mshambuliaji wake wa Argentina mwenye umri wa miaka 22 Lautaro Martinez in the summer. (Star)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic