February 5, 2020

UONGOZI wa Singida United umesema kuwa leo utapambana kupata ushindi mbele ya Biashara United kwenye mchezo wao utakaochezwa Uwanja wa Karume.

Singida United imekuwa na mwendo wa kusuasua msimu huu ambapo kwenye jumla ya mechi 18 ilizocheza imeshinda mechi mbili ikiwa nafasi ya 20 na imefungwa jumla ya mabao 26 na kufunga 8.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa mapito magumu yana mwisho wake.

"Tunapitia kipindi kigumu kwenye timu yetu, tunatambua mwisho wake unakaribia na tutafanya vizuri mashabiki watupe sapoti," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic