LICHA ya kwamba Simba inaongoza ligi hivi sasa, lakini beki kisiki wa timu hiyo, Pascal Wawa, amesema ishu ya kuanza kuwaza ubingwa bado sana kutokana na wachezaji kujipa kazi kubwa zaidi ya kufanya.
Simba ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ambapo msimu uliopita walimaliza ligi wakiwa na pointi 93. Kabla ya mechi yao ya jana Jumamosi dhidi ya Lipuli, Simba ilikuwa kileleni na pointi zake 53.
Wawa raia wa Ivory Coast, alisema kuwa wanatambua shauku kubwa ya mashabiki ni kuona timu yao inatwaa ubingwa, lakini jambo hilo halitokei haraka bila ya kujipanga kwa wachezaji katika kufikia malengo yao.
“Ni kweli tuna kazi ya kutetea ubingwa ila kwa sasa hatuwezi kusema sisi ni mabingwa tayari, bado tuna mechi nyingi za kucheza na ushindani ni mkubwa. Kupitia matokeo mazuri tutakayopata uwanjani yatafungua njia kwetu kupata kile tunachokihitaji,” alisema Wawa.
0 COMMENTS:
Post a Comment