February 24, 2020


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mpira sio sawa na rede una kanuni zake jambo ambalo wanapaswa walielewe mashabiki.

Yanga imelazimisha sare kwenye mechi nne mfululizo za Ligi Kuu Bara na kupoteza pointi nane kati ya 12 ilizokuwa inazisaka.

Ilianza kupata sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mbeya City kisha ikafuata 0-0 mbele ya Tanzania Prisons, 0-0 mbele ya Polisi Tanzania na sare ya 0-0 mbele ya Coastal Union.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema:-"Mpira una kanuni zake na kila timu inapambana kupata matokeo chanya, hivyo nasi tunapambana, Mpira sio sawa na rede. timu zinacheza, mashabiki waendelee kuipa sapoti timu.

Yanga imefunga mabao mawili kwenye mechi zake nne mfululizo ikiwa imefunga jumla ya mabao 25 baada ya kucheza mechi 22.

6 COMMENTS:

  1. No comments Mr.Nugaz, but learn to speak few words.

    ReplyDelete
  2. Haya matusi ndio yanafanya watu watake kumpiga. Hajui mpira halafu anajifanya mtaalamu. Yanga tubadilishieni huyu Bogus.

    ReplyDelete
  3. Sio wote wanaoingia chumba cha mtihani wankwenda kufanya mtihani,na sio wote wanaofanya mtihani watafaulu,dunia ni sehemu ya ajabu sana ila one day yes.NUGAZ WEWE BOGUS HUNDRED PERCENT.

    ReplyDelete
  4. BOGUS NI YULE ANAESEMA UKWELI AU YULE ANAEPOTEZA WATU MWELEKEO !!!
    KWA UPANDE WANGU HUYU NI MKWELI NA NI MTU SAHIHI KWA YANGA

    ReplyDelete
  5. NUGAZ ANAWEZA KUWA SI BOGUS NA ANAWEZA KUWA ANASEMA UKWELI ILA KWA KUTUAMBIA MASHABIKI KUWA ''MPIRA SIO SAWA NA REDE'' KAA HIYO ZARAU YAANI SISI HATUJUAGI MPIRA WA YANGA MPAKA ULIPOKUJA WEWE KUTUAMBIA MPIRA UNA KANUNI SIO REDE? HIVI KWELI KULIKUWA NA SABABU YA KUTUAMBIA HIVYO KAMA SIO KUTAKA KUTUUZI TU? HAYA LAKINI MASHABIKI TULICHANGIA YANGA YETU KWA HALI NA MALI. ZAHERA ANATUJUA SANA NGUVU YETU.

    ReplyDelete
  6. KAMA NUGAS SIO BOGUS BASI NINYI WASHABIKI NDIO BOGUS
    KASEMA MPIRA SIO REDE KUMBE HATA HAMJUI NINI REDE NA MPIRA NI8 NINI.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic