February 16, 2020


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa, mechi nne zijazo ambazo ni sawa na dakika 360, watazitumia kwa ajili ya maandalizi ya kuiangamiza Simba

Yanga ambayo jana Jumamosi ilipambana na Prisons kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, itapambana na Simba Machi 8, mwaka huu uwanjani hapo.

Kabla ya kupambana na Simba, itakuwa na kibarua cha kucheza mechi nne dhidi ya Polisi Tanzania, Coastal Union, Alliance na Mbao. Katika mechi hizo, mbili dhidi ya Polisi na Coastal ndizo watachezea ugenini. Zilizobaki nyumbani.

“Tuna mechi nyingi kabla ya kukutana na Simba na zote hizo ni ngumu, hivyo lazima tupambane kwa mpangilio mzuri, mechi hizo zitatupa hali ya kujiamini na kutengeneza kikosi maalumu kitakachotupa nguvu ya kuiangamiza Simba.

“Nafahamu kwamba huwezi kutengeneza kikosi bora iwapo utashindwa kuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo, kwa sasa nataka wachezaji wangu wacheze vizuri kabla ya mchezo huo na huwa ninawaambia kwamba silali kwa ajili ya kuwaza mbinu mpya za kushinda mechi zetu,” alisema Luc.

MIPANGO YA KUISHUSHA SIMBA

Katika hatua nyingine, kocha huyo amesema kuwa njia ya kuishusha Simba kutoka nafasi ya kwanza iliyopo sasa ni wao kushinda mechi zao zote zilizobaki.

Kabla ya mechi za jana Jumamosi, Yanga ilikuwa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 38 ikicheza mechi 19 na Simba ikiongoza ligi ikijikusanyia pointi 53 katika mechi 21. Tofauti yao ni pointi 15.

Baada ya mechi za jana, Simba imebakiwa na mechi 16 ambazo ni sawa na pointi 48, huku Yanga mechi zao 18 zilizobaki ni sawa na pointi 54.

Akizungumza na Spoti Xtra, Luc alisema kuwa ana mlima mkubwa wa pointi anazodaiwa na Simba jambo ambalo linamfanya apasue kichwa kufikiria namna ya kumalizana nao.

“Simba ni wapinzani wetu wakubwa ambao kwa sasa wapo nafasi ya kwanza, nimewaambia wachezaji wangu kwamba jambo moja tu litakalowashusha wapinzani wetu pale walipo ni sisi kushinda mechi zetu zote.

“Kushinda mechi zote zilizobaki inawezekana endapo wachezaji watafuata maelekezo ninayowapatia,” alisema kocha huyo.

Kauli ya kocha huyo iliungwa mkono na viungo wake, Papy Tshishimbi na Haruna Niyonzima ambao wameapa watashinda kila mchezo ulio mbele yao hadi mwisho wa ligi.

Niyonzima alisema: “Kwa sasa tunaangalia mbele kwa mbele, hatuna sababu ya kurudi nyuma, kule tulikotoka hatukuwa katika hali nzuri, ila kwa sasa timu ipo vizuri, wachezaji wote tuna morali ya juu. Kila mchezo tutacheza kama fainali ili tushinde yote.”

Naye Tshishimbi alisema: “Si rahisi kupata pointi tatu katika kila mchezo, lakini sisi tutapambana kuhakikisha tunatimiza malengo kwa kushinda mechi

9 COMMENTS:

  1. Unajua waswahili hasa wazee waliopita walituachia kauli ambazo vizazi vya sasa tunajitoa akili kutokujua maana yake. Wazee wanasema utavuna ulichopanda.Na hii ndivyo ligi ilivyo hivi sasa kwani katika timu zote ligi kuu bara ni Simba pekee iliyochukua jitihada za dhat pre season kukiandaa kikosi chao kwa ajili ya mashindano mbali mbali.Licha ya kelele nyingi kuwa labda Simba inabebwa lakini ukweli ni kwamba Simba wapo vizuri na walijiandaa kivitendo kupambana kwa ajili ya kutetea ubingwa wao. Azam Fc kama watachukua ubingwa isingeshangaza sana kutokana na jinsi timu yao ilivyojengeka ingawa walikosa pre season ya maana kulinganisha na Simba. Yanga kama watachukua ubingwa itashangaza sana kiasi cha kuwa maajabu kwani ukiangalia Yanga walipotokea huko ni timu iliokuwa imekumbwa na migogoro,ukata wa hali ya juu, usajili wa hovyo kwani karibu wachezaji wote ambao walitajwa kuwa ndio watakujakuwa moyo wa timu ndani ya Yanga hivi sasa hawapo. Yanga walikuja kujaliza wachezaji katikati ya ligi.kiuhalisia Yanga hivi sasa ndio wapo kwenye pre season na kama kufanya vizuri kwa timu yao watalazimika kuwa wastahamilivu mpaka msimu ujao. Yanga kujipa moyo kuchukua ubingwa msimu huu zidi ya Simba ni utani. Simba wana uwezo wa kuchukua ubingwa kihali na kimali,wana kikosi imara kwa miaka mitatu mfululiizo sasa,wana benchi la ufundi liloshiba kabisa, wana viwanja vya kufanyia mazoezi vya uhakika, timu kama hii kwa ligi kama yetu ya Tanzania haiwezi kupata matokeo mazuri halafu ukasema inabebwa. Actual kama utakwenda kupitia marejeo ya video za mechi za Simba tangu nwanzo wa ligi utagundua kuwa ni moja kati ya timu iliyodhulumika sana na maamuzi ya marefaree.kinachowasaidia Yanga ni kwamba wana mashabiki wa kutosha nje ya uwanja kuuaminisha umma kuwa wana timu nzuri lakini kiukweli, nuna, lia, garagara Simba wana timu iliyokamilika kwa mbali zaidi kulinganisha na Yanga na kama Simba watashindwa kutetea ubingwa basi ni uzembe wao wenyewe,sema Simba nao wana matatizo yao binafsi na hasa ile kasumba ya kuamini kuwa tmu yao ni bora zaidi na haistaili kufungwa kitu ambacho ni ujinga kwani siku zote mpira huwa hauna adabu kimatokeo hata real Madrid au Basa hufungwa na vitimu vya hovyo tu ila kuteleza sio kuangauka ni kitendo kinachokukumbusha kuwa makini na hatua zako. Kwa maoni yangu timu kama Coastal Union ya Tanga ni moja ya timu ya kuchungwa sana hata Simba wajihazari sana nao kwani ni timu inayoimarika kila siku zikienda mbele na inaweza kufanya maajabu mwaka huu.

    ReplyDelete
  2. Mhindi kasema "domo jumba ya maneno"

    ReplyDelete
  3. Waanike mipango mpaka ikauke na waweke makundi ya kulalamika na kupondana yasiyo na hesabu na ikiwa Mnyama anakata mwendo tisini na tano, wenye kukata sitini, vipi watamfikia na kumpita alietangulia

    ReplyDelete
  4. Hao ni vyura ni wajinga kandambili hao hawapo sawa msiangaike nao ndugu zangu hawajitambuwi wanabebwa wanapewa hadi penati hakuna timu hapo vyura hao wamezoeya kupiga kelele

    ReplyDelete
  5. Wakati Yanga anawazia kushinda mechi zake zote, Simba nae ana mpango kama huo. Hebu tutimize kwanza ndoto ya yanga, akishinda zote anakuwa na points 93, wakati simba akishinda mechi zake zote isipokuwa dhidi ya yanga anakuwa na points 101. Sasa hapo unamshushaje simba pale kileleni?

    ReplyDelete
  6. ni kitu ambacho hakiwezekan kuchukua ubingwa na point 93 wakat mwenzako anazo 101 labda hawa vyura waimbee simba ipokwe poit 10 na wao washinde zote

    ReplyDelete
  7. Vyura matata Sana. Leo wanasema Molinga Zito Sana hafai

    ReplyDelete
  8. Ni muhimu mnyama akaanza hesabu za kumsainisha Morrison Kwa ajili ya mechi za klabu bingwa za Africa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic