March 6, 2020


MSHAMBULIAJI wa Azam FC Andrew Simchimba amejifunga ndani ya klabu hiyo kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Nyota huyo inaelezwa kuwa alikuwa kwenye hesabu za mabosi wa Kariakoo, Simba waliokuwa wanahitaji kuipata saini yake kwenye dirisha dogo hivyo dili lao limeshatibuka.

Simchimba aliyekuwa anakipiga Coastal Union kwa mkopo na sasa amerejea Azam FC mkatba wake ulikuwa unameguka mwezi Septemba mwaka huu na kuongezewa kandarasi yake ya miaka mitatu atadumu hapo kwa miaka mitatu mpaka 2023.

Benchi la ufundi la Azam FC limekuwa likimwamini nyota huyo ambaye amekuwa akitimiza majukumu yake kwenye timu hiyo ya Azam FC.

Kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na Ndanda FC alifunga bao la kufutia machozi kwa timu yake na kuipa pointi moja ilipokuwa kwenye ziara ya nyanda za juu Kusini.

1 COMMENTS:

  1. Huu si usajili wa Simba kwa sasa ni uzushi.Nnaimani kabisa kama Simba watafuata maelekezo ya kocha wao katika kuziba mapungufu yanayojitokeza hivi sasa basi wanaweza kuwa na timu moja hatari sana na kutikisha caf champion league. Kocha sven anaonekana kuwa mweledi sana na mapungufu ya wachezaji wake mmoja mmoja na kwa asilimia 90% ya maelezo yake anakuwa yupo sahihi. Simba inahitaji mabeki kazi wawili kuzidi level ya mabeki wake wa kati wa sasa. Mchezo wa Azam ni kigezo tosha Simba kujitathmini juu ya mangufu ya beki yake. Simba vile inahitaji fowadi kazi asilia wa kati mmoja au wawili kuja kuwapa changamoto mpya akina boko na kagere na wakati huu ndio wakati muafaka kwa maskauti wa Simba kuhangaika kutafuta wachezaji hao. Wasisubiri mpaka karibu na mashindano ya caf ndio wanaanza kutafuta wachezaji hao kwani wakati huo kila timu huwa zinatafuta wachezaji na kupelekea wachezaji kuwa ghali zaidi na wengine huwa washakuwa booked na timu zilizoshtuka kushughulikia usajili mapema. Ila to be honest kocha wa Simba anaonekana anajua nini kinahitajika kwenye timu ili kuwa na ushiriki wa heshima champions league. Kumbuka alishachukua kombe la mataifa ya Africa akiwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Cameruni kwa hivyo sio kilaza kama watanzania wengi wanadhani.Ni kocha mwenye kuelewa vyema fitna la soka la Africa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic