March 5, 2020

AZAM FC jana imeshindwa kufuta uteja wake wa msimu wa 2019/20 mbele ya Simba kwa kukubali kichapo cha mabao 3-2 Uwanja wa Taifa.

Kwenye mchezo wa kwanza ambao uliwakutanisha Simba na Azam, matajiri hao walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na mfungaji alikuwa ni Meddie Kagere na jana Machi 4 walikubali kudufugwa mabao 3-2 huku Kagere akiwatungua pia bao moja la ushindi.

Ushindi wa Simba unawafanya wajikite kileleni wakiwa na pointi 68 baada ya kucheza mechi 26 huku wakiwaacha Azam FC nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 48.

Machi 8, Simba itakuwa na kibarua cha kumenyana na Yanga mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa huku wakiwa na kumbukumbu ya kutoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 mchezo wa kwanza.

Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa atawaandaa vijana wake kwa umakini.

5 COMMENTS:

  1. Wakianguka siku hiyo au kutokadroo ubingwa 100% wa Mnyama mkali au ipite miujiza ya aliyetuumba

    ReplyDelete
  2. Hata mnyama afungwe bado yanga ana kibarua kizito na kigumu sana,anadaiwa alama ngapi?yani labda simba apoteze michezo zaidi ya 7 ndio yanga achukue ubingwa na hapo hapo yeye ahakikishe hafungwi mechi hata moja kuanzia mechi ya simba nakuendelea.kitu ambacho hakiwezekani.

    ReplyDelete
  3. Simba kweli wameamua, kuna soka fulani linapigwa msimbazi ni la kitabuni aisee...kuna mistakes kidaogo tu kwenye ukabaji ni kama wanategeana vile au wanahisi wapinzani watakosea.. kweli kabisa yakirekebishwa hayo Simba ni moto wa kuotea mbali.. ile striking force yao ni balaa sana... Ngoja tusubiri 8/03....

    ReplyDelete
  4. Simba iache kutegeana jukumu la kukaba Ni la wote sio mabeki uvivu waache

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic