March 12, 2020

KIKOSI cha Simba jana kimemaliza hasira za kichapo cha bao 1-0 mbele ya Yanga ilichopokea Machi 8 Uwanja wa Taifa kwa kuishushia kichapo Singida United cha mabao 8-0 Uwanja wa Uhuru.

Simba ilianza kwa kasi kwenye mchezo huo na ilipachika bao la kwanza kupitia kwa Meddie Kagere dakika ya kwanza akimalizia pasi ya Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ alirudi kambani mara tatu dakika ya 25,41 na 71 kwa pasi ya Hassan Dilunga na alifunga hat trick yake ya kwanza msimu huu.

Mabao mengine yalifungwa na Deo Kanda dk 12 kwa pasi ya Shomari  Kapombe na dk ya 18,John Bocco alifunga bao dk ya 19 Sharaf Shibob dk 59 kwa pasi ya Deo Kanda.
Singida United ilimaliza ikiwa pungufu kwa kumkosa kiungo wao mkongwe, Haruna Moshi ‘Boban’ ambaye alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 52 kwa kumpiga kiwiko, Aishi Manula.

Ushindi huo ni wa kwanza mkubwa msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara ambao wameupata Simba msimu huu.
Simba inafikisha pointi 71 ikifunga mabao 63 ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu bara. 

Pia kinakuwa kichapo cha pili kikubwa kwa Simba kutoa Uwanja wa Uhuru ambapo iliifunga msimu wa 2018/19 Coastal Union mabao 8-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic