March 12, 2020


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa kuna mpango mkubwa wa kuwapiga chini wachezaji wake wote ambao hawana mchango mkubwa ndani ya timu.

Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael leo itakuwa uwanjani kumenyana na KMC mchezo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 25.

Akizungumza na Saleh Jembe, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wanawatazama wachezaji wote wa Yanga kwa wakati ili kujua aina ya wachezaji wenye mchango ndani ya kikosi hicho na wale wasiokuwa na mchango panga linawahusu.

"Tumefanya usajili mkubwa lakini bado kunawachezaji wengine wamekuwa na mchango mdogo kutokana na sababu mbalimbali, kwa sasa tunamaliza tathimini ikikamilika wengine wataaachwa ili kuendelea na maisha mengine," amesema.

Miongoni mwa wachezaji ambao wamepewa madili na Yanga na hawaonekani ndani ya uwanja ni pamoja na David Molinga, Ally Ally, Yikpe Gnamien, Erick Kambamba.

5 COMMENTS:

  1. Yanga ikifungwa huwa huwandiki au siyo andika sasa mlivyo aibishwa leo mgongo wazi wakubwa aibu yenu hiyo

    ReplyDelete
  2. Hamuandiki mkifungwa na kmc au hamukucheza leo aibu hata kuandika GONGO WAZI

    ReplyDelete
  3. Kama ni kweli wamepewa hayo mamilioni ahadi ya kumfubga Mnyama basi wanyanganywe kwani wameteremsha aibu ya mwaka. Kila kukicha kejeli za vyura zimekuwa nyingi na mpaka sasahivi yule muandishi kimya anashindwa na Kawa bubu. MABINGWA WA JADI NDIO BADO MMO KATIKA MBiO ZA KUTWAA AUBINGWA? Tuliokuwa hatupati usingizi

    ReplyDelete
  4. Tokea kupata hicho kigoli kimoja tulikuwa hatupati usingizi lakini mitaa yote kimya juu ya mvuwa zote vyura vimefyata na huku Namungo, Polisi na Azam zote zinakungojeeni kwa hamu

    ReplyDelete
  5. Unaambiwa furaha ya masikini haidumu ndicho kilichowakuta vyura fc walifurahi ila kilichowakuta Leo kimya na wanasema malipo yapo hapa hapa duniani hawajakosea malipo yao wameyakuta leo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic