March 12, 2020


LEO saa 10:00 Yanga itamenyana na KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

Yanga itaingia uwanjani ikijiamini baada ya kuvunja rekodi iliyodumu kwa miaka minne bila kuifunga Simba baada ya ushindi walioupata Machi 8 wa bao 1-0 kupitia kwa Bernard Morrison.

Rekodi zinaibeba Yanga mbele ya KMC kwa kuipoteza timu hiyo iliyopanda daraja msimu wa 2018/19 kwa kushindwa kusepa na pointi tatu kwenye mechi zote tatu za ligi walizokutana.

Yanga imeshinda mechi mbili msimu wa 2018/19 na sare moja kwenye mechi ya kwanza msimu huu 2019/20 kwa kufungana bao 1-1 walipokutana Uwanja wa Taifa.

KMC imeifunga Yanga mabao mawili huku yenyewe ikifungwa mabao manne ambapo mchezo wa kwanza kukutana ilipopanda daraja ilifungwa bao 1-0 kupitia adhabu ya faulo iliyopigwa na Feisal Salum mechi ya pili Yanga ilishinda mabao 2-1 na kuifanya isepe na pointi sita jumla na mechi yao msimu huu ilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa anawaamini vijana wake watafanya kazi nzuri itakayowapa pointi tatu.

4 COMMENTS:

  1. Mbona hamsemi kafungwa Yanga?😂

    ReplyDelete
  2. Wana kigugumizi. Sasa wataendelea kuzuumzia kichapo cha Simba au cha Yanga. Endelee kubeza na ikiwa hawajapewa hayo mamilioni basi wasipewe kwani ni aibu tupu HAHAHAA. Munamuona Mungu?

    ReplyDelete
  3. Mbona taarifa za YANGA kufungwa hamwandiki???

    ReplyDelete
  4. Kwa mara ya kwanza naona matokeo ya mabingwa wa jadi yameshindikana kuchapishwa na kuhusu mbezo wa kichapo cha Mnyama yameshafikia mwishoni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic