IMEELEZWA kuwa, mabosi wa Yanga wameamua kumkabidhi majukumu ya kukisuka kikosi kitakachoimaliza Simba, Machi 8 Uwanja wa Taifa Kocha Msaidizi wa timu hiyyo Charles Mkwasa.
Simba itakaribishwa na Yanga Machi 8 Uwanja wa Taifa wakiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2.
Habari zinaeleza kuwa tayari jukumu la kukipanga kikosi kitakachoimaliza Simba lipo mkononi mwa Mkwassa ambaye aliimaliza Simba walipokutana nayo mchezo wa mzunguko wa kwanza.
"Simba wanajua itakuwa kazi rahisi kwa kuwa wanatambua kwamba Kocha Mkuu Luc Eymael hawatambui, kilichokubaliwa kwa sasa ni kuona majukumu yote kuhusu Simba, Mkwassa anayafanya.
"Kwenye ile sare ya mabao 2-2 Mkwassa ndiyo alikuwa shujaa sasa mchezo wetu unaofuata ni lazima pia tumpate shujaa wa mara ya pili," ilieleza taaarifa hiyo.
Eymael amesema kuwa wanachokifanya benchi la ufundi ni kufanya kazi kwa kushirikiana.
Huyo Mkwasa kuwepo Yanga ndio chanzo cha Yanga kufanya vibaya. Nakama Yanga wataingia na mbinu zile zile za Mkwasa za mechi ya kwanza kwa kocha huyu wa Simba jinsi alivyo mwepesi wa kusoma mchezo basi Yanga wataondoka na kilio. Na hapana shaka Yanga kukabidhiwa Mkwasa kwenye mechi ya simba ni maelekezo ya kamati ya ushirikina kwakuwa Mzungu asingekubaliana na upumbavu huo.
ReplyDeleteUlietoa maelezo hayo uko tim gani!!? Pilipili ya shamba yakuwashian?
ReplyDeleteHakuna timu hapo ndio tunachukuwa ubingwa wetu kwa kuwafunga hao kandambili aka vyura 3.
ReplyDeleteWacha tuone kitatokea nini ila kila la kheri yanga
ReplyDeletemachi 8
mbona umetoa siri sasa?
ReplyDeleteSaykoloji hiyo dhidi ya Mnyama ya kujifurahisha, ya kitoto na kujidanganya. Mna penik kubwa Sana hebu tulieni mbona Mnyama kimyaaa hapapatiki. Mbio za sakafuni huishia ukingoni
ReplyDelete