March 6, 2020


FRANCIS Kahata, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa wana kazi kubwa na ngumu ndani ya Ligi Kuu Bara kusaka pointi tatu kwa kuwa ndiyo malengo waliyojiwekea.

Kahata amekuwa kwenye ubora wake ndani ya Simba baada ya kujiunga msimu huu wa 2019/20 akitokea klabu ya Gormahia ya Kenya amehusika kwenye jumla ya mabao 10 ya Simba kati ya 55 akifunga mabao manne na kutoa pasi za mwisho sita.

Kahata amesema: "Kuna kazi kubwa ya kufanya ndani ya ligi, mechi zimekuwa ngumu na ushindani ni mkubwa lakini hatuna namna ni lazima tupambane kupata pointi tatu na hayo yote yanawezekana kwa kuwa tunashirkiana.

"Kushindwa kufikia malengo inaumiza na hilo lipo wazi, tunaomba sapoti ya mashabiki kwani wao wanatupa nguvu," 

Machi 8, Simba itakaribishwa na Yanga Uwanja wa Taifa kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara ikiwa ni mzunguko wa pili, kwenye mchezo wa kwanza waliocheza Januari 4, timu zote zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

3 COMMENTS:

  1. Tazama Hawana tabia ya kuropokwa kabisa taratibu na kuzistahi timu zote Bila ya kutaja mamilioni walioahidiwa kwasababu hii ni siri yao na mamilioni wao si mageni kwao wameshayazowea

    ReplyDelete
  2. Vita ya maneno inaumiza sana kuliko vita ya silaha kama panga na bunduki,chakujivunia kwa simba wamepata ngao(PSYCHOLOGICAL STATE) wamepikwa kuelewa nakusoma jinsi yakukabiliana na hali kama hiyo,natoa pongezi kwa waalimu,rai kwa shabiki wa simba "ENDELEEN KUA WAPOLE NA WASTARAABU MAANA MTAJIKUTA MMESHINDA VITA KUBWA SANA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic