March 6, 2020


HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wataongeza ulinzi kuelekea kwenye mechi yao ya Simba inayotarajiwa kufanyika Machi 8 Uwanja wa Taifa.

Bumbuli amesema kuwa sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuongeza usalama na kutunza siri zao kabla ya kukutana na watani zao wa jadi.

"Tunatambua kwamba kuna kazi ngumu ambayo ipo mbele yetu lakini tumejipanga na tulichokifanya kwa sasa ni kuongeza ulinzi ndani ya timu ili kukwepa yale mambo yasiyo ya kitimu kufanyka kwetu.

"Morali ya wachezaji ni kubwa na kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.

Yanga iliyo chini ya Luc Eymael itakutana Simba iliyotoka kushinda mabao 3-2 mbele ya Azam FC huku wao wakiibamiza Mbao FC mabao 2-0 zote zilicheza Uwanja wa Taifa.

4 COMMENTS:

  1. ONGEZENI ULINZI VYUMBANI PALE TAIFA WASIJE KUNYUNYIZIA VILEGEZA MWILI.

    ReplyDelete
  2. Ujinga mtupu. Mkinyunyiziwa mtaweza kuamka.Hizo dawa zinaitwaje?Kama sio uzushi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usipaniki bro au wewe ndo unatumwaga kupulizia dawa

      Delete
  3. Hizo hofu na panic mlizokuwa nazo ndizo zitazosababisha magoli ya chapchap na kuyakosa hayo mamilioni ambazo wengi wameshazipangia kulipa madeni madeni yao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic