March 1, 2020


IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa KMC leo anaingia uwanjani na kikosi chake akiwa na hofu tupu juu ya kibarua chake ndani ya timu hiyo.

KMC leo itamenyana na Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 2:00 usiku uwanja wa Taifa.

Habari zinaeleza kuwa mabosi wa KMC wamempa onyo Harerimana Haruna ambaye ni kocha Mkuu kuhusu hatma yake ndani ya kikosi hicho ambacho mwendo wake ni wa kusuasua.

Haruna amesema:'' Ninafanya kazi kwenye mazingira magumu kwa sasa wachezaji ni wakorofi hawafuati maelekezo na nina mashaka na kibarua changu kwa sasa,".

KMC ipo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 21 imecheza mechi 24.

1 COMMENTS:

  1. Nakuom wa duwa ushinde mechi ijayo sio hii ya leo ya Simba lakini ya baadae

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic