March 6, 2020



UONGOZI wa Yanga na mdhamini GSM wameahidi kutoa Sh milioni 200 kwa wachezaji wa Yanga iwapo watashinda mechi yao dhidi ya Simba Jumapili, Machi 8, kwenye Uwanja wa Taifa.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema wadhamini wa GSM wameweka mezani Sh200 Milioni kwa wachezaji endapo watapata ushindi wa aina yoyote siku hiyo. 


“Hata wakichukua ubingwa sio tatizo, tunachohitaji ni kuwachapa, nadhani raha ya ubingwa utakuwa umeisha na kuwanyamazisha kupiga kelele hovyo mtaani.

 “Tulikuwa na utaratibu wa kutoa motisha kila wanaposhinda kwenye michezo ya Ligi Kuu hupewa Sh 10Milioni, lakini kutokana na umuhimu wa mchezo wa Jumapili tumeamua kufanya kitu kwa wachezaji ili kuweka raha Jangwani,’ amesema.

4 COMMENTS:

  1. CHAKUWASHAURI TU NDUGU ZANGU KWA NAMNA YOYOTE ILE JUMAPILI LAZIMA MPIGWE,ILA KAMA MNATAKA KUSHINDA KWA KUTUMIA PESA BASI NUNUENI MECHI MBONA JAMBO DOGO SANA,MPENI JAMAA MILION 200 HIZO ILI MUIFUNGE SIMBA THEN HATA KOMBE PIA TUTAWAPATIA KAMA MKILITAKA,KULIKO KUAIBIKA KUTAKAKO WAKUTA JUMAPILI,NI MAONI NA USHAURI TU MUWE NA MAANDALIZI MEMA YA JUMAPILI.

    ReplyDelete
  2. Nakuunga mkono tutawauzia hilo kombe ama wamuhonge refa ili washinde rais wa cuf yupo uwanjani jumapili wataona cha moto kandambili aka vyura wa jangwani hao

    ReplyDelete
  3. Huyo gsm ache kuongeza mtaji wa kuuza mataulo na mashuka awape nyingi kandambili milioni 200 ndoto hizo matangazo hayo

    ReplyDelete
  4. Mpeni na salehe jembe ili azidi kuwasifia zaidi awandike kwenye gazeti lenu la champion

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic