March 6, 2020


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa kuelekea mchezo wao wa Jumapili, Machi 8, Uwanja wa Taifa dhidi ya Yanga wachezaji wake lazima wacheze kwa juhudi ili kupata matokeo mazuri.

Sven alisimamia dabi ya kwanza Januari 4, alikasirishwa na kitendo cha wachezaji wake kukubali kutunguliwa mabao mawili ndani ya dakika saba kwenye sare ya kufungana mabao 2-2 baada ya Simba kuanza kushinda mabao mawili.

Raia huyo wa Ubelgiji amesema:" Wachezaji wote kwa pamoja ninaamini wanatambua uhitaji wa mashabiki na uwezo wao uwanjani ni mkubwa ninaamini watacheza vizuri ili mashabiki pia wafurahi.

"Endapo watacheza kwa juhudi itakuwa rahisi kupata ushindi na mashabiki pia watafurahi kuona timu ikicheza," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic