BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amefunguka kuwa kuifungia timu yake bao mbele ya Simba kumempa heshima na furaha kwa mashabiki wa Yanga.
Raia huyo wa Ghana alifunga bao hilo kwenye mchezo wake wa kwanza wa dabi uliochezwa Machi 8 Uwanja wa Taifa na Yanga ilishinda bao 1-0.
Morrison amehusika kwenye mabao sita kati ya 31 ya Yanga ambapo amefunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao.
"Furaha kubwa niliona kwa mashabki namna walivyofurahi na namna walivyonipokea hakika ilikuwa ni siku nzuri kwangu, wachezaji wenzangu na mashabiki kiujumla.
"Ninaona kwamba kila shabiki anapenda kupata matokeo mazuri lakini hayaji bila kushirikiana na kufanya yote kwa upendo hvyo wazidi kuwa pamoja nasi kila wakati," amesema.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa kutokana na kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.
Hakuna heshima hapo,ukitaka uonekane mtu saidia timu ipate ubingwa kama kweli unataka uonekane mtu,hapo umepotea brother.
ReplyDeleteYani tangia mibahatisha hiyo goli 1 la faulo basi ni kila siku ya mungu huyo salehe ni kuandika storry hiyo hiyo hadi mwisho wa dunia itakuwa akili nywele
ReplyDeleteWajinga ndio waliwao kwani hiyo YANGA ni matambara matupu hivi sasa.Vurugu tele yaani wameharamika kuibomoa timu yao kisa kuifunga simba labda mganga hajapata mgao waliomuahidi pia kama wanavyosusa baadhi ya wachezaji wao.sasa kiuhalisia sio muuaji wa Simba bali ni muuaji wa Yanga kwani ameshaleta fitna kubwa ndani ya Yanga mpasuko kuanzia wazamini,wachezaji hadi viongozi,Na hii inaonesha kiasi gani Simba ilivyo bora zidi ya Yanga katika kila maeneo kuanzia uongozi hadi wachezaji kwani ushindi wa goli moja la Yanga zidi ya Simba ni kama vile Yanga wamechukua ubingwa wa nchi hawaachi kuweweseka kulakukicha .
ReplyDeleteSaleh sasa imetosha. kila kukicha ni morison morrison utafikiri yeye ndie wa kwanza kuifunga Simba. Au mmekosa cha kuandika? Au kwa vile Yanga imebahatisha kuifunga Simba ndio imekua nongwa!!? Tumechoka na stori ya morrison kila siku
ReplyDeleteMWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA,AMEIFUNGA SIMBA HATIMAE ANAIBOMOA YANGA,KWANINI MOTISHA ISIGAIWE KWA WACHEZAJI WOTE INA MAANA MECHI YA SIMBA NA YANGA INA POINT NYINGI KULIKO MECHI NYINGINE?SASA KWANINI MECHI ZA YANGA NA SIMBA TU NDIO MNAWEKA MOTISHA ALAFU KWA WACHEZAJI WACHACHE?HILO NDILO KOSA MLILOFANYA NA HAPO NDIOMANA BAADAE WACHEZAJI WANAKUJA KUGOMA ILI WALIPWE STAHIKI ZAO NAKUSABABUSHA SIRI NYINGI SANA KUJULIKANA,ACHENI UJINGA,MOTIVATION MUST BE GIVEN TO ALL PLAYERS OF THE TEAM NO MATTER HOW THEY SUCRIFICE THEMSELVES OR NOT BUT FOR ALL,HII NDIO ILIYOSABABISHA MPASUKO YANGA NA BADO SANA MTAPASUKA PAAAAAAAAAAAAAAAAAAA.
ReplyDelete