March 28, 2020


PAPY Tshishimbi, nahodha wa Yanga amesema kuwa nafasi waliyoachwa na Simba kuwafikia kwa sasa kunahitaji juhudi na akili nyingi kutokana na mzigo wa pointi wanazodaiwa na idadi ya mechi walizonazo.

Tshishimbi amesema ni ngumu kuifikia Simba kwa sasa kwa pointi labda itokee wapoteze mechi zao zilizobaki na wao washinde mechi zao zilizobaki jambo ambalo anaona ni mtihani mgumu kufanikiwa hivyo amekubali yaishe kwa upande wa ubingwa.

Yanga ipo nafasi ya tatu na pointi 51, tofauti ya pointi 20 na Simba yenye pointi 71. Yanga imebakiwa na mechi 11, Simba mechi kumi.

“Haitakuwa kazi rahisi kuyafikia malengo ya kutwaa ubingwa kutokana na mambo yalivyo kwa sasa ila inaweza kutokea kutokana na mchezo wa mpira kuwa na matokeo tofauti labda ikishindikana sasa itakuwa wakati ujao.

"Wapinzani wetu wametuacha kwa pointi nyingi hilo linatoa nafasi kwao kutwaa ubingwa tena labda sisi tujipange kwa wakati ujao," amesema.

Ligi Kuu Bara kwa sasa imesimama kutokana na kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona na inatarajiwa kurejea baada ya mwezi mmoja.

4 COMMENTS:

  1. Njoo huku kijana uje uone mpira unavyochezwa,acha kupoteza muda una soka zuri sana la kimataifa sasa hapo yanga utacheza kimataifa na nani?labda uisaidie timu ipate kombe la azam.hata huyo morison amekosea sana kutua yanga maana inaonekana soka lake limeshuka sana unawezaje kutoka kwenye timu zinazocheza kimataifa ukacheze kwenye timu ambazo hazina mashindano yoyote ya kimataifa?this is mistakes he made.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kila ubongo na mawazo yake,hukatazwi kuwaza pumba maana mikia kwa kujitoa ufahamu hamjambo. Kila unachokifanya wenzenu washafanya kitambo. Kweli maskin akipata ma..... hulia mbwataaaa,we

      Delete
  2. Tshishimbi hana uwezo wa kucheza Simba yenye malengo makubwa Africa. Ukimsajili huyo tegemea yaleyale ya miaka yote.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic