March 12, 2020

HITIMANA Thiery Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa timu yake inapambana kwa hali na mali kupata matokeo chanya bila upendeleo wowote.

Thiery amekiongoza kikosi chake kwenye mechi 27 kipo nafasi ya nne kikiwa na pointi 49 kibindoni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakionyesha juhudi kwenye mechi zote wanazocheza jambo linalowapa matokeo licha ya kupitia kwenye ratiba ngumu ya kusafiri.

"Tumekuwa tukipata matokeo mazuri wakati mwingine mabaya lakini yote yanatokana na juhudi za wachezaji wangu sipendelewi wala sibebwi na yeyote yule, sapoti ya mashabiki ni kubwa na tunabanwa na ratiba hasa kusafiri kunaleta uchovu kwa wachezaji,'" amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic