March 12, 2020


MSHAMBULIAJI wa Mtibwa Sugar, Salum Kihimbwa atakaa nje ya uwanja kwa muda wa siku 14 akitibu majeraha yake ya kifundo cha mguu.

Kihimbwa alirejea uwanjani hivi karibuni akitoka kutibu majeraha na aliumia Machi 7 kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Gairo, Morogoro.

Jana hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza na Polisi Tanzania na kulazimisha suluhu mchezo uliochezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi.

 Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 13 imecheza mechi 28 ina pointi 32 kibindoni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic