March 4, 2020











HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa anawaamini wachezaji wake watapambana mbele ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa leo utakaochezwa Uwanja wa Gairo, Morogoro.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa anajivunia uwezo wa wachezaji wake kupambana ndani ya uwanja jambo linalompa matumaini ya kupata matokeo mbele ya Mtibwa Sugar.
“Tupo vizuri na wachezaji wangu wamekuwa wakionyesha uwezo ambao unanishangaza licha ya kupitia kwenye ugumu wa ratiba hasa kusafiri kunatufanya tucheze chini ya uwezo wetu ambao tunao ila tutapambana bila kuchoka,” amesema Thiery.
Namungo FC ipo nafasi ya nne ikiwa imecheza mechi 24 imejikusanyia pointi 46.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic