March 11, 2020


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa vijana wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho utakaopigwa Uwanja wa Taifa dhidi ya KMC.

Yanga itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 1-0 mbele ya Simba lililofungwa na Bernard Morrison kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa Machi 8.

Eymael amesema:"Kila mchezaji yupo tayari na ari ni kubwa kuelekea mchezo wetu wa unaofuata ushindi mbele ya Simba umeongeza morali imani yetu wachezaji watafanya vema mashabiki watupe sapoti.".

Yanga kwenye mchezo wa kwanza wa msimu huu mbele ya KMC ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1

5 COMMENTS:

  1. Heeee wewe uandishi gani huu...toka lini Luc Eymael akawa kocha wa Simba ?

    ReplyDelete
  2. Eti Eymael ni Kocho wa Simba,kweli waandishi wetu ninyi mrudi shule tuu

    ReplyDelete
  3. Lisemalo lipo kama halipo linakuja

    ReplyDelete
  4. Wapi palipoelezwa Eymael kocha wa Simba? Au mlitaka iwe hivyo?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic