HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wataongeza ulinzi kuelekea kwenye mechi yao ya Simba inayotarajiwa kufanyika Machi 8 Uwanja wa Taifa.
Bumbuli amesema kuwa sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuongeza usalama na kutunza siri zao kabla ya kukutana na watani zao wa jadi.
"Tunatambua kwamba kuna kazi ngumu ambayo ipo mbele yetu lakini tumejipanga na tulichokifanya kwa sasa ni kuongeza ulinzi ndani ya timu ili kukwepa yale mambo yasiyo ya kitimu kufanyka kwetu.
"Morali ya wachezaji ni kubwa na kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.
Yanga iliyo chini ya Luc Eymael itakutana Simba iliyotoka kushinda mabao 3-2 mbele ya Azam FC huku wao wakiibamiza Mbao FC mabao 2-0 zote zilicheza Uwanja wa Taifa.







ONGEZENI ULINZI VYUMBANI PALE TAIFA WASIJE KUNYUNYIZIA VILEGEZA MWILI.
ReplyDeleteUjinga mtupu. Mkinyunyiziwa mtaweza kuamka.Hizo dawa zinaitwaje?Kama sio uzushi?
ReplyDeleteUsipaniki bro au wewe ndo unatumwaga kupulizia dawa
DeleteHizo hofu na panic mlizokuwa nazo ndizo zitazosababisha magoli ya chapchap na kuyakosa hayo mamilioni ambazo wengi wameshazipangia kulipa madeni madeni yao
ReplyDelete