MAKAMU Mwenyekiti wa Klabu ya
Alliance, Stephano Nyaitati amefunguka kuwa uongozi wa klabu hiyo umekuwa
hauingilii majukumu ya makocha kama inavyodaiwa.
Hii inakuja kutokana na ile
tabia ya kufukuza makocha kila wakati na hivi karibuni waliokuwa makocha wa
timu hiyo, Felix Minziro na msaidizi wake Wandiba alidai kuingiliwa
katika majukumu yake.
Nyaitati amesema:“Kuna taarifa kwamba uongozi wa
Alliance chini ya Mkurugenzi wake James Bwire zinadai tumekuwa tukiwaingilia
makocha kwenye majukumu yao ukweli ni kwamba sisi huwa hatufanyi hivyo ndiyo
maana tumekuwa tukileta wataalamu na yanapotokea mabadiliko yanakuwa ya kawaida
sana hivyo isitafsiriwe vibaya"
"Makocha wengi wakipigwa chini kutokana na uwezo wao mdogo ama sababu nyingine wamekuwa wakisema
mkurugenzi wetu anaingilia katika majukumu yao naomba ieleweke kwamba
hatuwaingili kwenye majukumu yao bali tumekuwa
tukifanya mabadiliko ya kawaida ambayo kimsingi huweza kufanywa na klabu
yoyote,”amesema Nyaitati.
Kwa msimu huu tu, Alliance
imewatimua Athuman Bilali, Habib Kondo, Malale Hamsini na, Fred Felix Minziro.
Chanzo: SpotiXtra








0 COMMENTS:
Post a Comment