ALEEM Alibha Kaimu Mwenyekiti wa Pamba SC inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza amesema kuwa kwa sasa mpango mkubwa uliopo ni kuboresha mikataba ya wachezaji wao ili kupunguza presha wakati wa dirisha la usajili utakapofika.
Pamba kwa sasa ipo nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza Kundi B ikiwa na pointi 22.
Alibhai amesema:“Tumepanga kuwaongezea mikataba
baadhi ya wachezaji wetu ambao wamekuwa wakipambana kwenye timu
yetu na kuonekana msaada mkubwa ili kuelekea usajili wa dirisha kubwa
tusihangaike kupata wachezaji.
“Wapo wachezaji wenye umri mdogo na wamekuwa wakifanya vizuri hao tutawapa kipaumbele kikubwa lengo
ikiwa ni kuhakikisha kwamba tunaiboresha timu," .







0 COMMENTS:
Post a Comment