April 16, 2020


KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison amesema kuwa kama mabosi wa Simba wangemalizana na meneja wake basi angesaini jumlajumla kwa watani hao wa jadi ila haikuwezekana.

Morrison alikuwa anawindwa na Simba ambao walikuwa wanahitaji huduma yake baada ya kugundua kwamba alisaini kandarasi ya miezi sita alipotua Bongo.

Kiungo huyo amesema:"Mchezaji mzuri anajulikana kutokana na kazi yake ndani ya uwanja, Simba walikwama kuzungumza na meneja wangu ambaye niliwaelekeza baada ya wao kuonyesha nia ya kunitaka.

"Labda kama wangekubaliana na meneja wangu huenda ningecheza Simba ila wao walishindwa kufika mwisho kwani hilo suala nililiacha mikononi mwa meneja wangu," amesema.

Baada ya kutua Bongo mechi yake ya kwanza ilikuwa mbele ya Singida United na alitoa pasi yake ya kwanza ya bao lililofungwa na kiungo mwenzake, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda wakati Yanga ikishinda mabao 3-1.

3 COMMENTS:

  1. Naaam naona Leo umetuletea habar ya swahiba wako Morrison angalau umepunua

    ReplyDelete
  2. Ha ha ha ha ha ha eti mambo yangekua sawa,kwani hayako sawa??bado unaiota simba brother pole sana,simba sio level yako wewe baki huko uendelee kupoteza uwezo wako maana unashindana peke yako sasa utaachaje kushinda?Ajibu ameshindana pekeake unajua kilichompata?ALIFUNGA MAGOLI 7 NA ASIST 16,kwanini simba hafanyi hivyo?kwasababu simba kuna vigongo wengi sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic