RAIS wa klabu ya Barcelona, Josep Maria
Bartomeu amesema msimu ujao klabu hiyo itafanya usajili bora ambao
hautategemewa.
Kuelekea msimu ujao Klabu ya Barcelona imekuwa
ikihusishwa kusajili nyota wengi wakali huku ikielezwa kuwa na mpango wa kumrejesha Neymar Jr ndani ya Barcelona.
Akizungumza
na Mundo Deportivo, rais alisema: “Kwa sasa siwezi kusema ni nani ambaye tutamsajili msimu ujao, ila
tunahitaji kuwa na wachezaji bora.
Kiongozi huyo alisema licha ya uwepo wa Virusi vya Corona bado mipango yao ipo
palepale kwenye usajili wao.
“Mipango
yetu bado, Abidal na wenzake wanaendelea kupambana japo najua msimu
utakuwa mgumu kwa upande wa fedha
kutokana na uchumi kuyumba.
Hata hivyo, ripoti kutoka nchini Hispania
zinaeleza kuwa Barcelona imekuwa ikipambana katika kuwanasa Neymar na Lautaro.
Imeelezwa kuwa Barcelona kitendo cha kutaka
kumrejesha Neymar basi itawagharimu kiasi cha euro milioni 180, Huku Barca
inataka kulipa kiasi cha euro milioni 70 kumnasa Lautora pamoja na Arturo Vidal.
Barcelona kwa sasa inapambana kuhakikisha ina
imarisha safu yao ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inamtegemea Messi kwani
Suarez na Dembele wametupwa nje kutokana na majeruhi.








0 COMMENTS:
Post a Comment