April 22, 2020


WAKALA wa straika wa Simba, Meddie Kagere, Patrick Gakumba, amefunguka kwamba dili la straika wake kutakiwa na klabu ya Hispania limekuwepo na kitu pekee ambacho kinakwamisha suala hilo ni mabosi wa mchezaji wake, Simba.

Gakumba ameongezea kuwa alipata dili hilo la Kagere la kutakiwa na moja ya klabu ambazo zinashiriki Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) ambapo walikuwa wanamhitaji straika huyo mwenye mabao 19 kwenye Ligi Kuu Bara.

Wakala huyo amesema kuwa alipata dili hilo baada ya kuzungumza na rafiki yake ambaye anaishi Hispania ambapo alikuwa anataka ampeleke straika huyo kwa ajili ya mkopo ambao angeweza kununuliwa moja kwa moja.

“Rafiki yangu anayekaa Hispania ndiye ambaye aliniambia kuwa moja ya klabu za ligi kuu ya nchi hiyo inamtaka Kagere kwa ajili ya mkopo na kama akifanya vizuri basi angeweza kusajiliwa moja kwa moja.

“Kwa sasa wao wanasubiri majibu kutoka huku ambapo ishu kubwa ni suala la mkataba wake na Simba na wao ndiyo ambao wanashikilia dili hilo.

“Nilizungumza nao na wao kwa sasa wanasikilizia juu ya hilo, ni dili ambalo kama litashindikana litanifanya nikose fedha nyingi,” amesema.

Chanzo: Championi

Licha ya jina la klabu hiyo kufichwa, inaelezwa kuwa ni Levante ndiyo inayomhitaji straika 

5 COMMENTS:

  1. Upumbavu mtupu apelekwe kwa mkopo? Yaani mchezaji anamkataba na simba halafu simba wamtoe bure kwa mkopo kwa kutegemea kuwa eti atanunuliwa ili simba inufaike na mauzo fikirisho au hewa kisa uisipania? Faridi wa azam hadi leo anasota. Yaani ukisoma hii makala unaona kabisa huu ni utapeli. Yaani ni dili zile zile za kibongo bongo. Kama simba wanataka kumuuza kagere basi watamuuza kwa pesa cash tena nyingi tu hapa hapa Africa. Umri ule wa kagere sio wa kwenda kucheza kwa mkopo ili kiwango kikipanda ndio anununuliwe walikuja Sevia ya Hispania hapa na walishangaa uwezo wa wachezaji wa simba na kukiri kuwa wengi wa wachezaji wa simba wana level ya kimataifa kwa maana yakwamba waliwazidi uwezo hata baadhi wachezaji wa Sevia. Wakati mwengine ndipo pale unapoona mwanataaluma wa kiafrica aliebobea anakwenda kufauata ushauri pumba na wa kijinga kutoka kwa mtu asiejua hata anachokiongea kwa kuwa tu mtu huyo ni mzungu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acheni polojo aende wapi huyo babu umri umekwenda atamalizia soka hapohapo hirizi fc

      Delete
  2. Hawa wa nafikiri Simba mabwege. Wanamtaka kwa mkopo kwani hawajui kuwa Simba ina wenyewe na Kgere Ana mwenyewe na wala si mfanya kazi wa ndani. Eti kwa mkopo

    ReplyDelete
  3. Kagere amezaliwa mwak 1986nkwa mujibu wa Google, kama ni kweli umri wake hadi 2020 utrakuwa si chini ya miaka 34, hivi ni kweli bado anatakiwa la liga? Nadhani isijekuwa zile mbinu zetu za kupandisha signing fee unapofika muda wa mkataba mpya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hizo porojo tu kagere na umri wake na la Liga wapi na wapi, tusidanganyane

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic