April 22, 2020



YIDAH Sven, kiungo anayekipiga ndani ya Klabu ya Kariobang Sharks ya Kenya amesema kuwa anavutiwa na uwezo wa kiungo Papy Tshishimbi na Fei Toto ambao wanakipiga Yanga jambo ambalo litampendeza akiungana nao.

Sven alipata nafasi ya kucheza na wachezaji hao kwenye mchezo wa siku ya Wanachi Uwanja wa Taifa ambapo ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Kwa sasa inaelezwa kuwa mabosi wa Yanga wanaiwinda saini ya kiungo huyo ambaye anakaribia kumaliza mkataba wake ndani ya Sharks.

Sven amesema:"Nipo tayari kutua ndani ya Klabu ya Yanga kwani ni timu kubwa ambayo kila mmoja atapenda kucheza bila mashaka yoyote.

"Ninawatambua baadhi ya viungo wanaokipiga Yanga ikiwa ni pamoja na Fei na Tshishimbi hawa wapo vizuri nitafurahi iwapo nitapata nafasi ya kucheza nao," .

4 COMMENTS:

  1. Huyu ni pro wa ishirini na mbili anaetajwa kutua yanga,napata kigugumizi kuhusu usajili wa yanga mbona inaonekana kama kuna ubabaishaji sana,haiwezekani wachezaji wa kigeni wanafika ishirini na zaidi kwanini?ngoja tusubiri tuone.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani Yanga ndo wanataja kuwa tunamtaka huyu na huyu au waandishi uchwara

      Delete
  2. Staili yao walivyowasajili kina Balinya....Na usishangae kusikia Lionel Messi naye yuko kwenye rada zao za kusajiliwa na Yanga.

    ReplyDelete
  3. si kweli kuwa hao wte n wanatakiwa na yanga. bali ni magazeti yamekosa kupata habari makini wanaishia kuparusa taarifa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic