KOCHA
wa klabu ya Espanyol ya La Liga, Abelardo Fernandez amesema kuwa mpaka sasa wana watu 10 ambao wameathirika na Virusi vya Corona.
Katika wagonjwa
hao 10, wachezaji nane wa kikosi cha kwanza nao wamekuwa ni kati ya
watu kumi ambao wameambukizwa Virusi vya Corona.
Wachezaji nane
wa kikosi cha kwanza pamoja na makocha wawili ndiyo ambao wamepata
maambukizi ya Virusi vya Corona.
Kocha
huyo amesema: “ Ndani ya klabu ya Espanyol tuna kesi 10 za maambukizi ya Virusi
vya Corona , wachezaji nane wa kikosi cha kwanza na makocha wawili.
“Mambo
ni magumu kutokana na hali halisi ya sasa na hatujui
hata hatma ya ligi ikoje na hapa tulipofika hata ligi ikirejea bado
hali za wachezaji hazijawa sawa na kila mtu anatamani kurudi uwanjani," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment