April 16, 2020


INAELEZWA kuwa miongoni mwa nyota wazawa ambao wanakubalika ndani ya Simba ni hawa wazawa wanne ambao ni Salum Abubakar,'Sure Boy', anayekipiga Azam FC, Dikson Job anayekipiga ndani ya Mtibwa Sugar, Bakari Mwamnyeto anayekipiga ndani ya Coastal Union na Lukas Kikoti anayekipiga ndani ya Namungo.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven amesema kuwa anahitaji kupata wachezaji wazawa ambao wanauwezo  mkubwa na umri mdongo huku akilitaja jina la Kikoti anayekipiga ndani ya Namungo.

Sure Boy wa Azam FC kwa sasa yupo kwenye hesabu za mabosi wa Yanga ambao wanahitaji kumuongeza ndani ya kikosi hicho.

Job amesema kuwa amekuwa akiskia habari za kuhitajika ndani ya Simba ila suala hilo analiachia uongozi wa Mtibwa Sugar ambao wanamsimamia kwa sasa.

Nondo amesema kuwa hana mashaka na uwezo wake ni suala la makubaliano tu ili ajiunge na Simba iwapo wanahitaji saini yake.

1 COMMENTS:

  1. NYIE VYOMBO VYA HABARI NDIO MNAZUSHAZUSHA MAMBO NA TETESI ZA UONGO HALAFU BAADAYE VIONGOZI WA KLABU WANAINGIZWA MKENGE KUJIBU TETESI....HEBU ACHENI MARA MOJA KAMA HAKUNA HABARI NYINGINE ELIMISHENI RAIA KUHUSU CORONA NA NAMNA YA KUJIKINGA KULIKO KUTAFUTA UMBEA NA UONGO KWENYE USAJILI ILI KUMKUZA MCHEZAJI NA KUZIINGIZA KLABU KWENYE NAFASI YA KUKANUSHA AMA KUTETEA HABARI...ILI WAONGOPE NA KUTOA KAULI HALAFU WAINGIE KWENYE MATATIZO


    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic