ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Swedy Mkwabi ameitaka Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo kushughulikia masuala yote ya muhimu ikiwemo kuhakikisha Sh. bilioni 20 zinawekwa kwenye akaunti.
Mkwabi amesema Simba ndani ya uwanja haina shida kwa kuwa inakwenda vizuri, kilichobaki ni kwa bodi inayoongozwa na Mohammed Dewji ‘Mo’ ishughulikie mambo ya nje ya uwanja ambayo yataonekana na mashabiki.
Mkwabi aliwahi kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, aliyepata nafasi ya kuiongoza Simba kwa muda mfupi, kisha baadaye akaamua kujiondoa kwenye nafasi hiyo kwa kile kilichodaiwa kuwa na mgogoro wa chini kwa chini na Mo.
Akizungumzia ishu hiyo, Mkwabi alisema ipo haja ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba kushughulikia masuala ambayo yapo nje ya uwanja yanayoonekana kwa mashabikina wanachama,huku akisisitiza kuwa moja ya vitu vya msingi ni kuhakikisha ile Sh bilioni 20 aliyoahidi Mo inawekwa kwenye akaunti kama ambavyo mwekezaji huyo aliahidi.
“Simba haina shida ndani ya uwanja, kama matokeo inapata na ina wachezaji wazuri, kwa sasa sipo kwenye uongozi wa klabu hiyo, lakini nazungumza kama mwanachama na Mwanasimba, niiombe Bodi ya Wakurugenzi kuhakikisha inashughulikia masuala mbalimbali yatakayojenga klabu nje ya uwanja, ikiwemo Sh bilioni 20 kuwekwa kwenye akaunti ya klabu kama ambavyo Mo aliahidi wakati anataka uwekezaji,” alisema Mkwabi.
Suala hilo la Sh bilioni 20, liliungwa mkono na Mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage ambaye naye alipoulizwa alisema: “Kama kweli Mo hajaweka hizo katika Fixed Account ya klabu atakuwa anafanya makosa, kwa sababu ni kitu ambacho aliahidi na Wanasimba wanatakiwa kuona hilo linatekelezwa, watu wa Simba pia hamtakiwi kukaa kimya, semeni ukweli kama mnaona mambo hayaendi vizuri.”
Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda ili azungumzie ishu hiyo ya Sh bilioni 20, ambapo alijibu kuwa: “Hayo mambo wala sisi hayatusumbui, tunachoangalia ni kufikia malengo na kuyafikia mabadiliko ya kiuendeshaji, kuhusu Sh bilioni 20, kwa kifupi tu zilishawekwa kwenye akaunti na bado hazijaanza kutumika kabisa.”
Chanzo Championi
Kaduguda ni mweupe kichwani hizo pesa zinatakiwa zichajiwe na riba maana aliikopesha simba
ReplyDeletemijitu mingine sijui ikoje. wanaona utulivu umetamalaki simba wanaanza kuleta majungu yao.
ReplyDeleteMo hamia katika uwekezaji wa timu ya vijana,waachie hao timu ya wakubwa.
ReplyDeleteKuna mijitu inatamani Simba ifanane na yebo yebo, eti atakuwa Mo anafanya makosa, mbona hamuhoji pesa za uwanja na mishahara kuingizwa kwa wakati inatoka wapi!! Wakati nyie mkiwa viongozi uwanja uliwashinda, leo mnaanza majungu, eti msikae kimyaa, Kaduguda chapa kazi, acha wale waliojiondoa wateseke.
ReplyDeleteUtulivu, amani, fikra pevu, na malengo ya muda mrefu viwe vipaunbele Simba. Pesa anazotoa Mo mbonavh huyu x-mwenyekiti hahoji? Vision, vision ndugu x-chair!
ReplyDeleteHakika mpira wa bongo hauwezi kwenda na hasa kama tutataka uendeshwe na wafanya biashara. Nyasi walinunua club, uwanja walinunua wanachama leo hii mtu kutandaza tu anawaambia bill 5 na bado tunakubali. Leo hii kaduguda kwa njaa zake unaudanganya umma kuwa tayari bill. 20 ziko kwenye fixed account huku akijua sio kweli.
ReplyDeleteInashangaza sana kuona wadau kushapalia bilioni 20 za muwekazaji mwenye hisa 49% kama zimewekwa kwenye bank account ya klabu.Kaduguda anasema ziliwekwa lkn mtu anapinga hazijawekwa.Hiyo sio kumtendea haki muwekazaji kwani ni bodi ya wakurugenzi wanaopaswa kutamka hilo na mmoja wa wakurugenzi wa bodi hiyo Kaduguda amedhibitisha zimewekwa lkn wadau tunasahau kuwa hivi matumizi ya pesa kama mishahara ya wachezaji, benchi la ufundi,watendaji,usafiri zinatoka wapi? Ktk hisa za wanachama 51% wamesha contribute kiasi gani
ReplyDeleteMkwabi na Rage wacheni majungu hayo!!! fanyeni yanayowahusu
ReplyDeleteTafadhali wale wanaohoji hizo pesa wstafute gazeti la mwananchi la tarehe 25/07/2019 wasome maagizo ya waziri kuhusu uwekezaji
ReplyDelete