April 6, 2020


JAMES Kotei, kiraka wa zamani wa Simba amesema kuwa iwapo mabosi wake wa zamani watahitaji saini yake hana tatizo nao kwani hawakuzinguana.

Nyota huyo kabla ya kusepa ndani ya Simba aliibuka kuwa kiungo bora wa timu kwa msimu wa 2018/19 walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

"Ubora wa Simba hakuna ambaye anaweza kugoma kufanya kazi kutokana na ushirikiano uliopo na ukizingatia kwamba sikugombana na viongozi.

"Iwapo itatokea kila kitu kimekwenda sawa nitarudi kuvaa jezi ya Simba kazi yangu ni mchezaji sichagui kambi," amesema. 

 Baada ya kusepa Simba aliibukia Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa sasa anakipiga ndani ya Belarus.

2 COMMENTS:

  1. Huyu anaonyesha anapenda kucheza simba. Kama uongozi unaona bado anahitajika ni vyema wamrudishe huyu badala ya kuhangaika na Okwi ambaye nionavyo mimi yeye anajali maslahi zaidi

    ReplyDelete
  2. uzuri wa kuotei anacheza mpaka beki huyu ni kiraka kama nyoni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic