MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa wazawa wana uwezo mkubwa wa kucheza nje ya nchi ila wanashindwa kujiamini na kujituma ndani ya uwanja.
Kwa sasa Ligi Kuu Bara ikiwa imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona, Kagere ametupia mabao 19 akiwa ni namba moja kwa utupiaji.
Kagere amesema:" Wachezaji wazawa hasa kwa nafasi ambayo ninacheza ya ushambuliaji wana nafasi ya kufanya vizuri na kuwa bora ila kinachowakwamisha ni kwamba wanashindwa kujiamini na kufanyia kazi makosa yao wanayoyafanya ndani ya uwanja.
"Ikiwa wataongeza juhudi na kufanya kazi kwa kujituma itakuwa rahisi kwao kutusua na kufikia malengo ambayo wamejiwekea.
"Nafasi yao kwao kutoka nje ipo lakini lazima wasikubali mafanikio ya muda mfupi yatawafanya wasifikie malengo waliyojiwekea," amesema.








Yeye amecheza wapi zaidi EAC!? Mbona hajajiamini akacheze SA au NA!? Amekuta wabongo kichefuchefu tu. Hana tofauti na Okwi, mpira wao bongo tu
ReplyDeleteHao ndio walewale wa siku zote
ReplyDeleteAmecheza Tunisia. Wewe kama umemjua Kagere leo kaa kimya.
ReplyDeleteWewe ndo umejua mpira ukubwa ukubwani, Kagere amecheza ligi gani amecheza? hivi unaweza sema Okwi na Kichuya wamecheza Tunisia na Misri mtawalia? Acheni kujidanganya, kuna kwenda na kucheza. Alienda ES Zarzis mwaka 2012 na mwaka huohuo akarudi police ya kwao baada ya maisha kumshinda. Ana tofauti gani na Ngasa kwenda Westham united au Lunyamila kwenda ujerumani. Sio lazima kila kitu ujibu, kama huna takwimu kalale
DeletePeleka ujinga huko.Kagere amecheza Tunisia 2012 akarudi Polisi nä wakaenda HK Tirana ya Albania mwaka 2014 mpaka 2015 akasajiliwa na Gör Mahia. Kagere amewakimbiza 2018/19 kwa kuwa mfungaji bora na anaendelea kuwakimbiza kwa kuongoza katika ufungaji tena kwa mbali. Terminator ni fowadi wa mfano hapa Bongo.
ReplyDeleteWe ndo mjinga, lete takwimu amecheza mechi ngapi!? Alienda 2012 akachemka na msimu uliofuata akaja kucheza police. Ana tofauti gani na kichuya au Okwi alivyoenda Tunisia!? Tatizo mnaongozwa na roho badala ya akiri ndio maana mkaitwa mbumbumbu
DeleteTatizo mnakariri ,angalien hata cv yake
ReplyDeleteCV yake iko wazi na hata ukiingia website ya hiyo timu inaonyesha walimsajiri msimu was 2012 na msimu was 2013 akarudi kucheza timu ya police Rwanda. Tatizo watu wana mapenzi yaliyopitiliza kiasi kwamba hawataki kukubali ukweli
DeleteTatizo mnakariri ,angalien hata cv yake
ReplyDeleteEti maisha yalimshinda Tunisia!Utafikiri anaye comment ni mke wake. Alicheza msimu mmoja akarudi Police FC.Ajabu yake nini?Kuna mjinga analinganisha nä Mrisho Ngassa na West Ham au sijui Lunyamila Ujerumani hata timu haijulikani.Hao walicheza hata kwa mkataba wa nusu mwaka?
ReplyDeleteKagere ni mfano wa mchezaji anayejituma ambaye mafowadi wazawa wanabidi wamuige.
Tatizo hauna hoja ndio maana unakimbilia kutukana, wewe unayemtetea ni mke wake, kaolewe basi!! Kusajiliwa na kucheza ni vitu viwili tofauti. Hakucheza, ndio maana jamaa hapo juu kawambia leteni takwimu alicheza mechi gani? asingeweza sajiliwa mara mbili ndani ya msimu mmoja. Mtakuwa mbumbumbu hadi lini?
DeleteKagere weka mbali na Morisoni
ReplyDelete