April 4, 2020


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa beki wa Simba Yusuph Mlipili anatakiwa kuongeza juhudi ili kupata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza.

Mlipili ndani ya Simba msimu huu hajawa na nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kutokana na kile kinachoelezwa ni ushindani wa namba ndani ya kikosi cha Simba.

Kwa sasa Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28 imebakiwa na mechi 10 kukamilisha mzunguko wa kwanza ila kwa sasa ligi imesimama kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona.

Sven amesema:"Bado kuna nafasi ya wachezaji wasiokuwa na nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kucheza ikiwa ni pamoja na Mlipili haina maana kwamba ni mchezaji mbaya hapana ni lazima aonyeshe utofauti na wengine kwani kikosi kina wachezaji wengi,".

4 COMMENTS:

  1. Kwa kuwa watu wengi wanalalamika kutopangwa kwa huyu kijana, ni vyema kocha angempa hata mechi moja mbili hata kama kipindi kimoja ili aonyeshe ujuzi/ ubovu wake ili mjadala ufungwe. Vinginevyo watu wanaamini kuna chuki binafsi.

    ReplyDelete
  2. Vipi utajulikana uwezo wake Bila ya kupewa nafasi za kweli. Huenda hakuonekana uwezo wake wakati wakujifuwa lakini akaonesha maajabu pale atapoaminiwa na kupewa nafasi za kikweli angalau kila mchezo angalau dakika kadha kuweza kujenga imani

    ReplyDelete
  3. Shida ya watanzania ni makocha wote mwalimu anasema mlipili angoze juhudi wanatokea wanywa pombe za kienyeji wanasema apangwe ina maana benchi la limewekwa la nini? punguzeni midomo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa hata mimi nashindwa kuwaelewa hasa wapenzi wa mpira wa hata TZ maana kama ni chuki iweje kila kocha aje akuchukie wewe? mbona hamchukii kenedy au Santos au wawa au Nyoni ila ni kwa mlipili badala yake kumpa mlipili mbinu za kufanya vizur ninyi mnatetea ubovu, mazoezi ufanye vibaya et mechi ucheze uwe mzuri sasa hiyo nafas itatoka wapi ya kukujaribisha kweye nafasi?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic